ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, December 7, 2013

STARS YAIUA UGANDA

Kilimanjaro Stars imefanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali ikiwa ni pamoja na kuivua ubingwa, Uganda, The Cranes.
 
Katika mechi iliyomalizika punde katika michuano ya Chalenji inayofanyika nchini Kenya, Stars imevuka kwa mikwaju 3-2 huku kipa Ivo Mapunda akiwa shujaa.
Ivo alifanikiwa kudaka mikwaju miwili ya  penalty, akianza kudaka wa Alucho kabla ya kudaka ya pili iliyopigwa na Sserunkuma anayecheza naye katika kikosi kimoja cha mabingwa wa Kenya, Gor Mahia.
Okwi na Kiiza walipata upande wa Uganda, lakini upande wa Stars, Samatta na Nyoni wakakosa. Waliofunga ni Kiemba, Yondani na Chuji.
Katika dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2, Stars wakianza kuongoza kwa mabao mawili ya Ngassa, lakini Uganda wakasawazisha kupitia Sserunkuma (Dk ya 16) na Martin Mpuga (dk73).

No comments:

Post a Comment