ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, February 26, 2014

UKOSEFU WA FIKRA CHANYA WA BAADHI YA WANACHAMA WA SIMBA SC,HUKUMU YAKE NDIO HII

Takriban mwaka wa pili sasa, mashabiki wa Simba wanaendelea kuangalia muenendo mbovu wa timu yao.
Mashabiki pamoja na wanachama wengi wao wanawalaumu wachezaji kuwa wao ndio haswa kiini cha timu kufanya vibaya,wanawadhihaki,wanawatukana na kuwaambia kila aina ya neno baya na hata wengine kufikia hatua ya kutaka kuwapiga wachezaji wao bila kujua nini tatizo.

Siwezi kuwalaumu sana ila nachowalaumu ni kitu kimoja tu,kwanini wanatoa hukumu pasipokuwa na hakika??
Kumlaumu mchezaji kuwa anaihujumu timu pasipokujua anaishi vipi au kipi anakosa ni dhambi ambayo ikiendelea itatuhukumu,ingawa Simba ina bahati ya kupata wachezaji wanaoienda timu yao,mwisho wa siku na wao watachoka tu.

Tatizo kubwa la Simba SC walilianzisha wanachama wa timu hii. Wanachama hawa pasiokuelewa au pasipokufahamu wakakubali kuingia mikononi mwa mwenyekiti ambaye afahamu majukumu yake ndani ya Simba SC BW Ismail Aden Rage.

Yawezekana labda ni kwa sababu ana majukumu mengi lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rage ndiye kiini cha tattizo.

Rage ilipaswa afahamu matatizo ya timu yake na sio kuja na hoja nyepesi eti kuwa yeye hachezi pale timu inapofanya vibaya., Ikumbukwe kuwa maandalizi ya mpira wa miguu popote pale duniani yaanaanzia nje na ndani ni utekelezaji tu.

Lakini wanachama hawalioni hili wao wanawalamikia wachezaji peke yao.

KAMATI YA UTENDAJI
Wengi ya wanachama hawafahamu hii kitu, binafsi naweza kusema hapa ndipo kila kitu kwa Simba SC,.
Siku chache zilizopita kamati yetu ya utendaji iliamuru kumpiga chini Rage ili angalau timu yetu ikae sawa,ni kweli lilikuwa wazo zuri ila tatizo njiac waliyopitia ilikuwa dhaifu.

Rage aliporudi alidai kuwa hatambui mapinduzi hayo, Kamati ikawa imetulia kana kwamba haijui nini cha kufanya wakati katiba ya Simba iko wazi.

Katiba inasema wazi kabisa kuwa kama wajumbe wa kamati ya utendaji watajiuzuru,basi automatically Mwenyekiti naye anapoteza hadhi ya kuwa kiongozi. wajumbe hawakufanya hili matokeo yake ni wapo kama hawapo.

Hii ni mbaya sana, ni wajibu wanachama kufahamu tuhuma za kwanza wapeleke kwa viongozi wao na si wachezaji wa Simba peke yao. Sana sana mnavunja ari yao tu ya kujiamini pindi pale wanapokuwa uwanjani na nyinyi mkiwa mnaangalia.

TUKUBALI TULIKOSEA KUCHAGUA,ACHA TUHUKUMIWE KWA DHAMBI ZA KUCHAGUA KIBAYA KATIKA TIMU YETI!

No comments:

Post a Comment