ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, March 3, 2014

KIEMBA;SIMBA SIO MBOVU KAMA WATU WANAVYOFIKIRI

Kiungo maridhawa wa timu ya Simba SC, amewataka wadau wote wa Simba kuacha mara moja fikra zao kuwa Simba hii ni mbovu kwani ONYO la mwisho linakuja.

Akiongea na blog hii muda mfupi baada ya kuisha kwa mtanange dhidi ya Ruvu Shooting ulioisha kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-2, Nahodha huyo wa sasa wa Msimbazi amesema kuwa huwa wanapata wakati mgumu sana kwa kuwa timu yao inakamiwa na timu zote zinazocheza ligi kuu Tanzania bara.

Simba ambayo kwa sasa ina mwendo wa konokono, inapitia katika wakati mgumu sana kwani mpaka hivi sasa haina matarajio ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment