ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, March 6, 2014

LOGA KITANZINI SIMBA SC

Hali ya sintofahamu imezuka katika uongozi wa Simba SC juu ya mustakabali wa kocha wa sasa wa timu hiyo Zdravko Lugarusic.

Hali hiyo inatokea siku chache tu baada ya kocha huyo ambaye ni raia wa Croatia kuomba apewe mkataba mpya na klabu hiyo ya mtaa wa msimbazi.

Ikumbukwe kuwa, kocha huyo mwenye shahada ya juu ya ufundishaji soka, alisaini mkataba wa miezi 6 tu ili kuweza kuinusuru Simba iliyokuwa ikizama ingawa hata hivyo Loga bado hajaonesha makucha yake.

Taarifa za ndani kabisa ambazo SPS imezinasa zinasema kuwa tayari timu moja wapo inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara inamuwinda kocha huyo kwa udi na uvumba.

Wakati hali ikiendelea hivyo, Zdravko Lugarusic anatarajiwa kuteua kikosi cha wachezaji kumi na nane ambao atasafiri nao kuelekea Mbeya tayari kabisa kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Prisons.

Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa taifa Simba SC ilifanikiwa kuwazamisha maafande hao kwa jumla ya goli 1-0 .

No comments:

Post a Comment