ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, March 6, 2014

SIMBA 18 KWENDA MBEYA MUDA MFUPI UJAO

Kikosi cha wachezaji 18 toka timu ya Simba kinatarajiwa kuelekea jijini Mbeya muda mfupi ujao tayari kabisa kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Prisons.


Kocha Zdravko Lugarusic, atachagua wachezaji hao dakika chache zijazo ambao ndio watakaokwenda kuhakikisha kuwa Simba inaondoka na points zote 3 katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

Wakati huo huo, katibu mkuu wa Simba SC Bw Ezekiel Kamwaga, ameuambia mtandao huu kuwa hatua ya pili ya utayarishwaji na uanzwaji rasmi wa kutengeneza pitch kwa ajili ya Simba itaanza tarehe 15 mwezi huu.

Utengenezwaji huo wa pitch utaendelea katika uwanja wa Simba SC uliopo maeneo ya Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment