ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, March 6, 2014

YANGA WAMPIGA STOP BIN ZUBEIRY

Katika hali ya kushangaza na isiyokuwa ya kawaida, klabu yaYanga ya jijini Dar es salaam, imeipiga rasmi STOP blog ya Bin zubeiry kuandika habari yoyote inayohusu klabu hiyo.

Hatua hiyo inakuja muda mfupi tu baada ya blogu hiyo kuripoti kuwa uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania umetoa mgao kiduchu tu kwa wachezaji hao baada ya kazi nzito walioifanya kuwafunga Mabingwa wa Afrika katika mechi yao ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati hali nchini Tanzania ikiwa hivyo, tayari kikosi chao kitakaowavaa Al Ahly siku ya jumapili kimewasili nchini Misri katika jiji la Cairo.

No comments:

Post a Comment