ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, March 6, 2014

TAMBWE AWASILI DAR ES SALAAM

Mshambuliaji aliye katika kiwango cha juu kwa sasa Afrika mashariki na kati Amissi Tambwe yupo jijini Dar es salaam SPS inakufahamisha.

Mrundi huyo mwenye hasira na nyavu za timu pinzani ambaye kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji katika ligi kuu ya Tanzania, amewasili leo hii akitokea katika nchi yake ya Burundi baada ya ruhusa ya muda mfupi kulitumikia taifa lake.

SPS ilifika katika uwanja wa kinesi, na kumshuhudia mtukutu huyo wa magoli akiwa pembeni kabisa akiwaangalia wenzake wakiendelea na mazoezi .

Wakati huo huo, kikosi cha Simba SC, kesho kinatarajiwa kuelekea mkoani Mbeya tayari kabisa kwa mechi dhidi ya Prisons.

No comments:

Post a Comment