ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, March 3, 2014

TAMBWE HATARINI SIMBA SC

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Amissi Tambwe yupo katika hali tete ya kubaki au kuachana na Simba Sc  SPS inakufahamisha.

Habari za uhakika zilizonaswa na blog hii zinasema kuwa, mkataba wa Amissi Tambwe ulikuwa wazi kabisa kuwa kama atafanya vizuri basi ataongezewa mshahara lakini kinyume chake wanamzungusha.
Tambwe ambaye anatokea Vital O ya Burundi, amekuwa na msimu wa kwanza bora kabisa ambao mpaka sasa amefanikiwa kufumania nyavu mara 19 katika mechi 19 alizocheza.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga umekuwa ukifanya mawasiliano na mchezaji huyo ili aweze kumwaga wino jangwani kwa gharama zozote zile huku uongozi wa Simba SC ukiwa kimya.

Ikumbukwe kuwa leo asubuhi,gazeti la mwanaspoti lilitoka na taarifa kuwa mshambuliaji huyo bora wa afrika mashariki na kati anatakiwa na klabu ya DC Motema Pembe.

No comments:

Post a Comment