ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, July 30, 2014

MKUDE HALI TETE MSIMBAZI,MWENYEWE ASEMA ATAREJEA KWA KISHINDO

Kiungo mkabaji wa Simba Sports Club Jonas Gerrald Mkude hali yake bado si nzuri.,Akiongea moja kwa moja kwa simu na blog hii, kiungo huyo amesema bado hali yake haijatengamaa kiasi cha kupelekea kushindwa kuanza kufanya mazoezi na wenzake."Hali yangu si nzuri, bado naendelea na matibabu,nitakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne zaidi kuanzia leo ila wanachama na wapenzi wa Simba SC watarajie mazuri zaidi mwaka huu" aliongeza mchezaji huyo.

Jonas Mkude, aliumia akiwa na Stars katika mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa Mambas wa msumbiji katika mchezo ambao ulioisha kwa Taifa Stars kulazimishwa sare ya goli 2-2.

Ikumbukwe kuwa, kiungo huyo nyota ndiye aliyeweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Simba Platinum Supporters 2013/2014 miezi kadhaa iliyopita, tuzo hiyo alikabidhiwa  na mlezi wa SPS Profesa Juma Athuman Kapuya ndani ya ukumbi wa Vinna Hotel.

Wakati huo huo, kiungo maridhawa wa Simba SC Willlium Lucian maarufu kama Gallas ameanza mazoezi mepesi leo hii bada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku 5 baada ya kuumia nyama za paja.

No comments:

Post a Comment