ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, August 14, 2014

CASSILAS WA MSIMBAZI AMVUTIA KASI IVO MAPUNDA

Goli kipa mpya wa Simba SC, Hussein Sharif Casilas amesema kuwa uwezo wa hali ya juu anaouonesha Ivo Mapunda unamfanya ajitume zaidi ili kocha mkuu wa timu hiyo aweze kumpa nafasi.

Kipa huyo ambaye amejiunga Simba SC akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alikuwa katika wakati mgumu baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Zdravko Logarusic kuwa na imani na Ivo Mapunda.

" Nitajitahidi sana, yeye ni mzuri ila nina imani tutafanya kazi ya pamoja yenye manufaa kwa klabu yetu" alimaza mchezaji huyo.

Simba SC ina kipa watu hivi sasa ambao ni Hussein Sharif, Ivo Mapunda na Manyika Peter ambao wamebaki baada ya kukatwa jina la kinda liliokuwa linakuja kwa kasi Abuu Ashim.

Wakati huo huo, kikosi cha miamba hiyo ya Tanzania leo kitawasili visiwani Zanzibar tayari kabisa kuweka kambi ya maandalizi katik mechi za ligi kuu Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment