Nikiwa
nimekaa na jamaa mmoj ambaye alionesha kabisa ana uchungu na Simba SC ,
akiwa ameukunja uso wa sura yake huku akilaumu uchezaji wa beki kisiki
wa Simba SC Donald Musoti.
Ghafla aliinuka na kuanza kwa matusi kisha akaendelea"Musoti aondoke,asajiliwe Kiongela,kwanza si kasema kapata timu uarabuni basi aondoke tu"
Hawa ndio mashabiki wa Simba SC, mashabiki ambao walikuwa wakimpigia makofi Musoti alipomuweka kwapani Mrisho Ngassa katika mechi ya kwanza tu ya Musoti ya Nani mtani Jembe, hawa ndio mashabiki wanaoipenda Simba SC bila kujua nafasi za wachezaji uwanjani, mashabiki ambao walikuwa hawaangalii mipira mingi ya juu kuelekea Simba SC ilidondokea kwenye kichwa cha mchezaji gani.
Hii ni aibu halafu ni dhambi ya soka, hili tatizo ndio maana unaambiwa kama hujui tulia watu wafanye kazi kuliko kupiga kelele mwisho ukaonekana kituko.
Hatuwezi kufika kama sisi wenyewe ndio tunakuwa wa kwanza kuwakatisha tamaa wachezaji wetu, inabidi tubadilike!

No comments:
Post a Comment