ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, August 18, 2014

REDONDO NI SOMO TOSHA KWA AKINA GALLAS

Ramadhan Chombo (Redondo)

Fundi huyu wa mpira analazimika kuacha soka wakati bado kijana mdogo sana...kwanini anaacha mpira? kwa sababu mfumo wa soka la Tanzania ndio ulivyo, hata ukiwaangalia wachezaji mafundi wa zamani utakubali tu soka la Tanzania ni lile,

Kwa wale ambao bado mnacheza na mnapata mshahara mzuri, ni muda wa kuangalia mbali zaidi, ni muda wa kumfata Samatta alipo ili Simba ijivunie, ni muda wa kumuangalia kwa makini Mwinyi Kazimoto ambaye alikuwa akipotea na kipaji chake maridhawa.

La muhimu ni kufahamu maisha ya soka hayahitaji kusubiri sana, tumikia soka ili likutumikie, pia potezea soka ili nalo likupotezee,

"Vijana" ndani ya Simba SC huu si muda wa kusubiri na kukaa benchi eti bado haujakuwa, inabidi upambane, pambana zaidi ya Thomas Ulimwengu ambaye hakuwahi kugusa uchungu wa ligi kuu Tanzania bara.

Kwa wanaojua ni dhahiri kuwa kijana wa soka katika Tanzania ni yule ambaye ana uwezo wa kucheza kwa wakati huo, lakini kwa wale wanaoitwa wakongwe basi ndio jua linapotea...

Salaam

No comments:

Post a Comment