ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, August 8, 2014

TWAHA NA KISIGA,JEZI NAMBA 10 SIO YA KUKAA BENCHI NDANI YA SIMBA SC

Mwaka 2013, mtoto mdogo mwenye asili ya nguvu nyingi za miguu kutoka Coastal Union anasajiliwa Simba Sc na kwenda kutambulishwa moja kwa moja klabuni, mtoto huyu anayecheza nafasi ya winga ya pembeni au hata kati kati moja kwa moja aliweza kufanikiwa kuikamata jezi namba 10, ni ukweli uliothabiti kuwa katika mechi chache alizochezea aliitendea haki kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje muda mrefu pale Bamba Beach wakati timu inajiandaa dhidi ya Yanga katika sare ya 3-3..huyu ni Ibrahim Twaha shekue au Messi wa miguu yote.

KUTOKA GAZETI LA CHAMPIONI

'Jezi namba 10 yazua utata Simba SC, wachezaji watatu wanaigombea ambao ni Kisiga, Kiongela na Twaha Messi, hata meneja Nico Nyagawa alipoulizwa alisema jezi apewe Kisiga"

USAHIHI KWA JICHO LILILO MAKINI

Siku zote ikumbukwe kuwa jezi ya mchezaji husika huweza kuipata kama na kama tu mchezaji ameikuta hiyo jezi haina mtu au ameongea na mchezaji husika....hivyo ni muhimu Kisiga, na Kiongela wamuombemchezaji husika ili awakabidhi kama atapenda kufanya hivyo,,,ikumbukwe pia kuwa jezi namba 10 sio ya kukaa bench ndani ya Simba SC, mchezaji inabidi aitumikie ili kuitendea haki,, nani asiyefahamu Okwi alikuwa akivaa jezi namba 25 ambayo mpaka sasa imegeuka kuwa lulu Simba SC,? Nani asiyefahamu kuwa Mafisango alikuwa akivaa jezi namba 30 ambayo ni lulu mpaka sasa Simba SC ingawa imestaafishwa?

Maana yake mchezaji yoyote anaweza kuifanya jezi yake kuwa yaa thamani zaidi na si jezi kumfanya mchezaji kuwa wa thamani, Lino Musombo, Komabil Keita, Danniel Akuffor hawa walivaa jezi zilizokuwa bora ndani ya Simba SC, lakini hawakufanya kitu..

Wachezaji Salaam zenu!

No comments:

Post a Comment