ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, August 4, 2014

WAMBURA KUUNGURUMA KESHO

Aliyekuwa mgombea wa Urais Simba SC kabla ya kuenguliwa Michael Richard Wambura, anatarajia kuongea na waandishi wa habari kesho baada ya kupokea taarifa za kufukuzwa uanachama wa Simba SC.

Akiongea na waandishi wa habari leo hii, amesema kuwa kesho kila kitu atakiweka wazi na la msingi watu watulie kwa sasa.

Michael Wambura jana jumapili alifukuzwa uanachama wake ndani ya Simba SC, baada ya kupatikana na hatia ya kuipeleka klabu ya Simba katika mahakama za kawaida.

Uamuzi huo wa jana, uliwazoa pia zaidi ya wanachama 70 ambao nao walikuwa na kosa kama hilo alilolifanya katibu huyo wa zamani wa chama cha soka Tanzania FAT kabla ya kuwa TFF.

No comments:

Post a Comment