ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, February 3, 2015

UWANJA WA BUNJU NA TAMTHILIA YA KUSADIKIKA SIMBA SC!



Mwishoni mwa uongozi wake BW Ismail Aden Rage, moja Ya vitu ambavyo vilimfanya shabiki/ mkereketwa / mwanachama wa Simba Sc kuwa na mvuto wa timu yake ni ujengwaji wa Eneo la uwanja wa Simba pale Bunju nje kidogo Ya jiji la Dar Es Salam!

Hali hii ilionesha dhahiri kuwa Jamaa ana kitu ambacho anataka kukifanya kwa ajili ya Klabu yetu ingawa hicho kitu alituahidi ila aliweza kukianza...,Ni kweli alichelewa sana mpaka akaanza mwisho lakini ukweli unabaki pale pale kuwa Rage aliweza kuanza Mchakato wa ujenzi wa uwanja wetu.

Rais Evance Aveva Kabla Ya kuingia madarakani aliahidi kuendeleza mchakato huo mara moja , Ndio Siku kadhaa baada ya kupata ridhaa Ya wanachama wa Simba Sc, tulishuhudia baadhi Ya wajumbe wa kamati Ya utendaji wakitembelea eneo letu..,

Ikiwa sasa unaelekea mwaka mmoja baada ya kuuchagua Uongozi wetu huu, hakuna kilichobadilika zaidi ya eneo la uwanja kurejea katika hali yake Ya kuwa eneo la msitu...,

Inauma sana kuona hali hii inatokea katika uongozi ulioaminika na maelfu ya wanachama wa Simba Sc,,,

Haijulikanani tatizo Liko wapi kwa kuwa mpaka sasa wanachama wa Simba Sc bado hawajarejeshewa mrejesho sahihi wa mchakato ule,...

Simba Platinum Supporters , Home Boys ni baadhi ya matawi ambayo yalionesha wazi wazi kusaidia mchakato huu hata kwa kuunganisha nguvu kwa wanachama wote kuweza kupata tofali kadhaa...,

Ni muda wa Rais Evance Aveva kuamka.. , ni muda rasmi sasa wa Simba Sc kuanza mchakato wa kutengeneza uwanja kabla ya muda wa viongozi wetu kuelekea mwishoni!,

Imetolewa na SPS tEAm!

No comments:

Post a Comment