ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, December 5, 2013

MANDELA AFARIKI DUNIA

BONDIA wa zamani na Rias wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amefriki dunia.
Bondia wa zamani; Nelson Mandela enzi zake za ubondia. Pumzika kwa amani shujaa wa Afrika
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema usiku huu kwamba 'baba wa Taifa' la Afrika Kusini amefariki akiwa na umri wa miaka 95.
"Taifa letu limepoteza mtoto wake mkubwa. Watu wetu wamepoteza baba",".
Pumzika kwa amani shujaa;  Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amethibitisha Nelson Mandela amefariki akiwa na umri wa miaka 95
Nation's greatest son: Nelson Mandela lifts the World Cup trophy in Zurich, Switzerland, after FIFA's executive committee announced that South Africa would host the 2010 World Cup soccer tournament. South Africa's 'Greatest Son' died Thursday at 95
Mtoto mkubwa wa taifa: Nelson Mandela akiwa ameinua Kombe la Dunia mjini Zurich, Uswisi, baada ya Kamati ya Utendaji ya FIFA kutangaza Afrika Kusini itaandaa Fainali za Kombe la Dunia za 2010.






Mandela (katikati) akiwa na bingwa wa zamani wa uzito  juu, Mmarekani, Mike Tyson, Jason Mandela kulia na Don King nyuma yake

Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa Julai 18, mwaka 1918 na ndiye rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. 
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi wa rangi Apartheid katika Afrika Kusini. 
Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. 
Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.

No comments:

Post a Comment