ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, December 5, 2013

LUGARUSIC AGUNDUA UDHAIFU SIMBA SC

'Rooney' agundua ubovu Simba SC, ambadili namba baba ubaya ....

Mcroatia kagundua udhaifu Simba SC:akiwaeleza nyota wake mazoezini.

KOCHA mpya wa timu ya Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic amegundua ubovu mkubwa katika kikosi cha timu hiyo, baada ya kubaini mapungufu kwenye upande wa mabeki na uzoefu mdogo kwa wachezaji wake wengi.
Mcroatia huyo ameanza rasmi mazoezi na timu hiyo tokea Jumatatu iliyopita jioni mara baada ya kusaini mkataba wa miezi sita kukinoa kikosi hicho, siku zote za hizo amewasoma wachezaji wake na kubaini mapungufu hayo kwa wachezaji wake.
Akizungumza na SIMBA PLATINUM SUPPORTERS jijini Dar es Salaam, Logarusic alisema mabeki wake wengi wana vimo vifupi kitu ambacho ni hatari sana kwa aina ya mabeki wa kisasa, kufuatia udhaifu huo hivi sasa anahitaji mabeki warefu katika eneo la mabeki wa kati, pia amegundua matatizo katika ukabaji kwa mabeki wake.
“Sifa kubwa ya beki wa kati ni kuwa mrefu jambo litakalomsaidia kwenye ukabaji wa mipira ya juu na kupambana vizuri na aina yoyote ya washambuliaji, akikosa vigezo hivyo hatakuwa beki mzuri katika eneo hilo, udhaifu huo nimeuona kwenye kikosi changu.
“Pia wachezaji wengi nilionao ni chipukizi, hivyo sitaweza kuwatumia wote katika kisosi changu nitawachanganya na wazoefu waliopo kikosini ilikutengeneza kikosi bora, kwani nikiwatumia wote siwezi kufikia mafanikio kwa sasa,” alisema Logarusic
Logarusic ametengeneza programu maalumu kwa mabeki wake kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuanzia mazoezi ya juzi jioni, lengo ni kuona wanakuwa katika kiwango bora kuelekea kwenye mechi ngumu dhidi ya Yanga SC, itakayopigwa Desemba 21 mwaka huu.
Katika hatua nyingine alisema kuna wachezaji hawastahili kuchezea kikosi hicho kutokana na ubovu wao, ambapo amedai klabu hiyo ni kubwa na inastahili wachezaji wenye viwango vikubwa, hata hivyo alishindwa kuwataja wachezaji hao.
Mcroatia huyo aliyebatizwa jina la ‘Rooney’ na mashabiki wa timu hiyo, amembadilisha namba beki wa kushoto wa timu hiyo Issa Rashid ‘Baba ubaya’ na sasa atakuwa akitumika katika winga wa kushoto, kikubwa amegundua ana uwezo mkubwa wa kushambulia kuliko kuzuia, pia kimo chake kidogo nacho kimepelekea maamuzi hayo.
Wakati huo huo, kwenye mazoezi ya juzi jioni wachezaji wawili walianza majaribio na timu hiyo, wote wakiwa ni mabeki wa kati, ambao ni Mkongomani, Kika Christopher aliyetokea timu ya FC Lupopo ya Dr Congo, ambaye amewahi kuchezea klabu za Mahindra United ya India na Ahli-Taiz ya Yemen, mwingine ni Joram Nasson anayetokea timu ya Lipuli ya Iringa.

No comments:

Post a Comment