ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, December 5, 2013

MATOLA RASMI SIMBA

Uongozi wa Simba chini ya kamati ya utendaji umekubali kumpa mkataba mpya wa kocha msaidizi, Selemani Matola.


Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Matola alifanya mazungumzo jana na uongozi wa Simba kujadili suala hilo.

“Wamezungumza jana na ikiwezekana leo au kesho Matola anaweza kumaliza kila kitu kwa kusaini mkataba,” kilieleza chanzo.
Awali, Kocha mpya wa Simba, Logarusic alionekana kuchukizwa na Matola kutoonekana mazoezini.

Lakini baadaye alielezwa kuwa anasubiri kuingia makubaliano kwanza na uongozi wa Simba kwa kuwa hakuwa na mkataba.

Matola ameanza kazi jana baada ya makubaliano hayo na uongozi.

No comments:

Post a Comment