ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, December 5, 2013

SIMBA PLATINUM SUPPORTERS KUMTEMBELEA KISAKA JUMAMOSI

Kundi la mashabiki wachache, wenye nia thabiti na Simba Sc la Simba Platinum Supporters, linatarajiwa kumtembelea kocha wa makipa wa sasa wa timu hiyo James Kisaka nyumbani kwake.


Kisaka ambaye anasumbuliwa na maradhi katika mguu wake , afya yake imeendelea kuyumba baada ya kupatwa na matatizo katika mguu wake, kiasi cha kupelekea kushindwa kufanya kazi zake za kila siku.

Kwa kutambua uwepo wake, na thamani yake, vijana hao wachache Huku wakiungana na wenzao, wameanzisha Kampeni maalum ya kumchangia kocha wao huyo , kwa kiasi chochote ambacho mwana Simba anaweza akapata au kwa msaada wowote.

Kwa yeyote anayeweza kuguswa na tatizo la James Kisaka , basi unaweza kutuma msaada wako kwa katibu wa kundi Hilo ambaye ni Abdallah Simba kwa namba ya Simu ya +255714222345 au +255767222336

Shukrani kwa wote!


No comments:

Post a Comment