ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, December 3, 2013

REDONDO AFURAHIA MAZOEZI YA LOGARUSIC

Kiungo wa Simba ambaye alionekana mtovu wa nidhamu pia na kushuka kwa Kiwango chake chini ya kocha wa zamani wa Simba Sc Abdallah King Kibaden, ameonesha kuridhika na kufurahishwa na Mbinu mpya anazofundishwa na kocha wake wa sasa Zdravko Lugarusic .

Akiongea na blog hii, Kiungo huyo Ramadhan Chombo Redondo, amesema kuwa Mcroatia huyo anaonekana kuwa ana Mbinu mbadala na za kasi ya Hali ya juu, kiasi ambacho kinaweza kikawafanya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Redondo alikumbwa na mkasa huo akiwa pamoja na wachezaji wenzake Henry Joseph, Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud.

No comments:

Post a Comment