ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, December 1, 2013

SIMBA KUANZA MAZOEZI RASMI LEO

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam, leo jumatatu inatarajiwa kuanza mazoezi rasmi katika kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Ikiwa chini ya kocha mpya kabisa, timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi yake katika uwanja wa kinesi jijini Dar.


Wakati huo huo, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba SC, NDG Sweddy Mkwabi, amesema kuwa uteuzi uliyofanywa na mwenyekiti aliyesimamishwa wa Simba Bw Aden Rage dhidi ya Michael Wambura ni batili.
Akihojiwa katika kipindi cha michezo cha radio one, Mkwabi amesema kuwa kikatiba Rage hakupaswa kumteua Wambura kwani nafasi iliyobaki ni kutoka kwa baraza la wazee tu katika klabu ya Simba.


Ingawa amekiri kuwa wajumbe wengi wanahitaji kufanya kazi na Wambura ila katiba ingefuatwa kwanza.







No comments:

Post a Comment