ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, December 1, 2013

CHANONGO AIUA SOMALIA

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba Haruna Chanongo , Leo amedhihirisha ubora wake baada ya kuibeba Kilimanjaro Stars kuifunga timu dhaifu ya ya Somalia.

Ilikuwa dakika ya 57, pale kiungo huyo alipoonesha ubora wake katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha raia wa Denmark Kim Paulsen.

Kiujumla timu ya Taifa ya Tanganyika, haijainesha kitu chochote kipya Kwani ilicheza mpira mbovu zaidi katika kipindi cha kwanza.

Stars itabidi imshukuru refarii Kwani dakika ya 72, penati ya wazi iliyopaswa kutolewa na refarii, iliota mbawa.

Ikiwa imejikusanyia alama nne baada ya mechi ya Leo, Kilimanjaro Stars inabakiwa na mchezo mmoja tu dhidi ya Burundi, kabla ya kumaliza hatua ya makundi katika muendelezo wa michuano ya Cecafa .

No comments:

Post a Comment