ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, December 12, 2013

STARS MAJANGA!


Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
NG’OMBE wa masikini hazai, huo ni msemo maarufu wa wahenga ambao leo umedhihirika Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya- baada ya timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kukosa hata nafasi ya tatu katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa na Zambia kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Wachezaji wa Zambia wakishangilia baada ya kuiua Stars

Kipa Ivo Mapunda alipangua penalti mbili za Wazambia, Justin Zulu na Kondwani Mtonga, lakini Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa na Nahodha Kevin Yondan wote wakakosa penalti zao zikiokolewa na kipa wa Chipolopolo, Joshua Titima.
Waliofunga penalti za Zambia ni Felix Katongo, Ronald Kampamba, Bronson Chama, Julius Situmbeko, Rodrick Kabwe na Kabaso Chongo, wakati za Stars zilifungwa na Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Katika mchezo huo, Zambia walitangulia kupata bao dakika ya 52 kupitia kwa Ronald Kampamba kabla ya Mbwana Samatta kufunga bao zuri mno dakika ya 65 akiisawazishia Stars.
Mchezo huo ulisimama kwa dakika sita, dakika ya 88 kufuatia Polisi kufyatua mabomu ya machozi wakipambana na mashabiki wa Kenya waliokuwa wanataka kuingia bure uwanjani.
Wachezaji walianza kuanguka mmoja mmoja kutokana na kuzidiwa na hewa ya mabomu, hivyo marefa wakasimamisha mchezo kabla ya kuanza tena dakika sita baadaye. 
Kwa matokeo hayo, Stars inaondoka Challenge ya 2013 na nafasi ya nne kama mwaka jana mjini Kampala, Uganda ilipofungwa kwa penalti pia na Zanzibar katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Imehamishwa Toka kwa BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment