ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, January 29, 2014

MEDIA ZINAPOJARIBU KUCHOCHEA MVURUGANO NDANI YA SIMBA SC KWA MANUFAA YAO

Katika takriban siku tano zilizopita, hadithi kubwa ndani ya Simba Sc na vyombo vya habari ni ile Hali ya kutoelewana Kati ya Beki kisiki Joseph Owino na Kocha mkuu Zdravko Lugarusic .

Hali hii inatokea wakati timu ya Simba Sc ikikabiliwa na michuano ya ligi kuu Tanzania bara.

Ni Hali ambayo ilifanya Baadhi ya wanaSimba kuaminishwa kuwa Lugarusic ni mkorofi hivyo hawezi kukaa na wachezaji wowote wale katika timu yake.

Hali hii imechochewa zaidi na Baadhi ya waandishi wa habari ambao Kwao kutafuta habari za uhakika ni dhambi kubwa sana. 

Wakati Jana majira ya saa 9.00 alasiri naongea na Joseph Owino, hakika alikuwa mtu mchangamfu na mwenye kutaka kufahamu kwanini nahitaji kuongea nae, kiukweli Owino alisikitika sana baada ya kumfungulia kurasa za Baadhi ya magazeti yenye kichwa cha habari eti Owino kupelekwa Simba B.

Ni Owino yupi wa kwenda Simba B? Owino alisajili kwa kuchezea timu B?
Hakika inahuzunisha lakini hakuna jinsi., Joseph Owino Jana majira ya saa 10.00 alianza mazoezi rasmi na wenzake na Leo ataendelea pia.

Kukosana kupo Sana Kama mpo watu wengi kwenye sehemu moja lakini wanachofanya waandishi wa habari wa Tanzania hakipendezi!

No comments:

Post a Comment