ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, January 23, 2014

MKUDE KUKOSA WABAYA WAKE JUMAPILI

Kiungo cha Simba Sc Jonas Gerrald Mkude anatarajia kuukosa mchezo wa jumapili dhidi ya Rhino katika uwanja wa taifa.

Kiungo huyo mkabaji wa Simba Sc, ataukosa mchezo huo kwa kuwa na kadi tatu za njano pia akisumbuliwa na Malaria kiasi cha kushindwa kufanya mazoezi na wenzake wiki hii.

Ikumbukwe pia, kiungo huyo anayeongoza kwa goli bora la mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara, ndiye aliyewalazimisha Rhino kuambulia pointi moja tu Kati ya tatu katika mechi ya  kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara iliyofanyika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment