ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, January 25, 2014

SIMBA VS RHINO HAKUNA KULALA LEO TAIFA

Simba Sc maarufu Kama ( The Reds) , Leo inashuka dimbani uwanja wa taifa kuwavaa maafande wa Rhino katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Katika mchezo huo wa kusisimua wa Leo, kikosi hicho cha Msimbazi kitashuhudia kuwakosa wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza wenye matatizo mbali mbali.

Wachezaji wanaotegemewa kukosekana Leo ni Jonas Gerrald Mkude ambaye ana kadi tatu za njano, wakati Joseph Owino amepumzishwa kwa sababu maalum.

Wakati Huohuo , kikosi hicho kinatarajiwa kuweka ingizo jipya la Gilbert Kaze katika mechi ya kwanza mzunguko huu.


No comments:

Post a Comment