Beki kisiki wa timu ya Simba SC Hassan Isihaka,amesema kuwa hakuwahi kusaini na wala hana mkataba wowote na African Lyon ya jijini Dar es salaam.
Pacha huyo wa kapteni wa muda wote wa Simba B Hassan Hatib, amesema kuwa taarifa zilizoenea leo hii kuwa mmiliki wa African Lyon Rahim Zamunda kuwa amemsainisha mkataba wa kiasi cha shilingi milioni 18, ni uzushi wa hali ya juu.." Sikiza kaka, ni kweli nilikuwa kwa mkopo African Lyon na Zamunda aliwahi kunipa milioni 1.5 za kukubali kujiunga nao, muda wangu wa kuitumikia klabu ile umekwisha, nimerudi nyumbani na kama ana uhakika amenipa mkataba na kiasi hicho cha pesa basi aweke wazi" aliongeza Hassan Isihaka akiongea na SPS.
Hassan aliibukia kutoka katika kikosi cha pili cha Simba SC, kilichokuwa kinanolewa na nahodha wa zamani wa Simba SC huku akiwekwa pacha wa Hassan Hatib hali iliyopelekea kikosi hicho kunyakuwa kombe la ABC Super8 ambalo wanalishikilia mpaka hivi sasa.
Wakati huohuo, kikosi cha Simba Sc leo kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment