Kiwango maridhawa kinachooneshwa na kiungo wa Simba SC , kimewafanya mashabiki wa Simba Sc kuchanganyikiwa kwa furaha.
Ikiwa ni mara ya kwanza kufanya mazoezi ndani ya uzi wa msimbazi baada ya kuondoka miaka kadhaa iliyopita, Shaaban Kisiga maarufu kama Marlone , ameonyesha kiwango cha hali ya juu hali inayopelekea kuzidisha ufinyu wa nafasi ya kucheza wa baadhi ya viungo wa timu hiyo. " Kisiga amerudi, ni kama amezaliwa upya, ni mwepesi na nafikiri Loga atafanya kazi yake kwa kiungo huyu" hiyo ni kauli ya mwanachama mmoja aliyejulikana kwa jina la Steven Bernald, akijibu swali la SPS muda mfupi baada ya kuisha kwa mazoezi katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Shaaban Kisiga amesaini mkataba wa mwaka mmoja Simba SC baada ya kocha Zdravko Logarusic kupendekeza atafutwe kiungo mwingine mzoefu atakayeweza kuhimili mikimiki ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.
No comments:
Post a Comment