ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, July 25, 2014

SIMBA SC INAPOGEUZWA BIDHAA YA KUJITANGAZIA SHAFFIH DAUDA, KABURU NAYE AINGIZWA KWENYE MKUMBO

Moja ya sifa kuu ya uandishi wa habari wa aina yoyote ni ueledi , Uweledi huu humfanya msomaji aelewe nini maana ya kitu anacholazimishwa akisome au akiangalie na hata kusikiza.

Siku hizi kumezuka mfumuko wa aina mbali mbali ya waandishi wa habari ambamo baadhi yao huifanya tasnia hiyo kudharauliwa.

Katika pita pita yangu leo nilibahatika kuingia katika mtandao wa shaffihdauda ambapo nilikutana na habari yenye kichwa kisemacho..MAGUMASHI, KABURU AZURURA NA SAAD KIPANGA KWENYE GARI YAKE AKILAZIMISHA SIMBA IMSAJILI"

Hapa ndipo waandishi wa habari wetu siku hizi walipofikia,,,moja ya kitu alichoongelea kuwa katika ripoti aliyoiacha Loga, hakuna jina la Saad Kipanga bali kuna jina la Elius Maguli. hii maana yake Shaffih Dauda aliiona ripoti ya kocha Zdravko Logarusic, je kama kweli ni nani alimuonesha Shaffih ripoti ya Logarusic?

Jibu ni mmoja au wengi ndani ya wajumbe wa kamati ya usajili.

Shaffih aliendelea kusema kuwa Kaburu aliwahi kusajili Abdallaah Juma na Paul Ngalema ambao hawakuhitajika na aliyewahi kuwa kocha wa Simba Milovan Cirkovic, matokeo yake viwango vimeshuka,,hapa namzungumzia yule Abdallah Juma aliyepiga hatrick ya pili msimu uliopita baada ya Amissi Tambwe akiwa ndani ya jezi ya Mtibwa Sugar,,kwa nini alaumiwe yeye?


Shaffihdauda amesahau kuwa Simba SC ina kamati ya usajili,,kumtupia lawama Geofrey Nyange ni kumuonea tu...wakati Nyange analeta wachezaji na kamati ya usajili inawakubali,,je tatizo ni la nani hapa?


Ikumbukwe kuwa , Shaffih huyu huyu aliwahi kuja na kauli mbili TATA, moja wapo aliwahi kusema kuwa KIEMBA AMESAINI YANGA, pia aliwahi kuja na kauli ya kusema kuwa LOGARUSIC ATIMULIWA SIMBA, je kuna lolote la ukweli hapo?


Ifikie wakati tuwe wakweli,,waandishi waandike na tuwaache makocha wafanye kazi yao!

No comments:

Post a Comment