ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, July 30, 2014

TFF WANAIHARIBU SIMBA SC, STARS NAYO INASUBIRI MUDA TU ILI IWEZE KUIGEUKA TFF

Moja ya ladha safi kabisa katika nafsi za watu wengi hapa nchini basi ni soka, nasema ni soka kwa sababu nimefanya uchunguzi wa hali ya juu na kugundua kuwa mchezo huo ni zaidi ya Burudani nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla.

Katika nchi yetu tumebarikiwa kuwa na wachezaji walio katika ubora wa hali ya juu na uwezo wa hali ya juu, ubora na uwezo wa ndio mara zote hufanya mchezo huu adhimu kupendwa na watu wa rika zote bila kujali jinsia zao.

Kama ilivyo kwa nchi nyingine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla, mchezo huu lazima uongozwe na chombo ambacho kina uwezo na sifa za kuongoza soka.

Sio siri kuwa Tanzania Football Federation yaani TFF ndio baba wa soka nchini, hali hiyo hufanya taasisi zote ndogo kisoka nchini ikiwemo Simba SC kufuata maagizo kutoka kwa baba yao yaani TFF.



Miaka kadhaa iliyopita wakati Rais wa TFF ni Leodger Tenga, wachezaji kadhaa waliitwa ili kuitumikia timu yao ya taifa kwa lengo la kuwawakilisha Watanzania katika mashindano mbalimbali Duniani yanayowakilishwa na mchezo huo. Mmoja wapo wa mchezaji aliyeitwa wakati huo alikuwa Kiungo mwenye jicho la kuona mbali Frank Domayo, ilipendeza kwakuwa Domayo alitii wito ule na alicheza kwa kiwango cha hali ya juu.

Miezi kadhaa mbele, kiungo huyo alipata majeraha kwenye mguu wake akiwa na timu ya taifa ya Tanzania, Daktari wa TFF walitambua hilo, na nafahamu hata Rais wa TFF na kamati yake walielezwa juu ya majeruhi waliopo Taifa Stars, je nini kilifata?

Haina shaka kuwa hakuna kilichofata zaidi ya kumkandakanda na barafu kwa kumpunguzia machungu bila kumpa tiba ya ugonjwa husika huku akiendelea kuitwa Stars ili aitumikie nchi yake, aliitwa na aliitumikia ila si kwa kiwango kile kile.

Mchezaji huyu aliyekuwa akitokea kwa waliokuwa mabingwa wa kandanda wa Tanzania bara yaani Yanga alizidi kuteseka pasipo kujua kujua kuwa anajiumiza au anaumizwa, Nna hakika kabisa kuwa nao Yanga waliambiwa kuhusu majeruhi ya mchezaji wao ila "walipotezea".Nini kilifata?


Kilichofata ni mchezaji kucheza katika kiwango cha chini kila kukicha na nafikiri ndio maana hata Yanga walishindwa kumpa mkataba mpya mpaka pale  Azam FC walipomchukua na kumfanyia vipimo na kugundua kuwa ana majeruhi ya muda mrefu, Domayo yupo katika tiba hivi sasa inayoshughulikiwa na uongozi wa Azam FC ambayo ilimnunua kama mchezaji huru,ikumbukwe kuwa mchezaji huyo aliumia akiwa Stars na alikuwa akiichezea Yanga kwa wakat huo.


Achana na Frank Domayo, kuna huyu mfalme wa Tanzania katika soka ambaye anamilikiwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye si mwingine bali ni Mbwana Ally Samatta.

Miezi kadhaa iliyopita, Samatta aliitwa kuja kuchezea timu ya taifa ya Tanzania, na kama ilivyokuwa kwa Frank Domayo, naye alipata majeraha ambayo yalimfanya awe nje kwa wiki kadhaa huku TFF ikijizungusha kumpa tiba inayotakiwa., kilichofata ni klabu yake inayommiliki kuja kumchukua na kwenda kumtibia kwa kuwa wanafahamu umuhimu wa Samatta katika aina ya soka la sasa.



Sahau kuhusu Samatta, kuna huyu kiungo fundi ambaye alikuwa SPS BEST PLAYER OFTHE YEAR 2013/2014 J onas Gerrald Mkude.

Kijana huyu chipukizi ambaye alikuwa nguzo ya timu ya Simba SC msimu uliopita nae anapitia njia za akina Domayo na Samatta huku TFF ikiwa imefumba macho.

Hakuna asiyejua kuwa mkude hayupo na Simba kwa sasa, hakuna asiyefahamu kuwa Mkude hajaanza mazoezi kwa sasa. Nini kinasabababisha asijiunge na wenzake?

Jibu ni rahisi tu, jibu ni kuwa kiungo huyu ana majeruhi katika kifundo cha mguu, majeruhi yale aliyapata wakati akijiandaa kuitumikia Taifa Stars katika kambi iliyowekwa Tukuyu jijini Mbeya.

Baada ya kupata majeruhi yale, TFF wao waliona ni bora arudi kwenye timu yake, hiyo ndio tiba ya TFF.

Uongozi wa Simba SC haukutaka kupambana na TFF bali imeamua kumtibu mchezaji wake wao wenyewe.. Mkude aliyeumia akiwa na Stars hatibiwi na TFF bali na Simba SC, je unategemea wachezaji wengine wa Stars wacheze vipi waki na uzi wa timu ya Taifa?

Muda utaongea!


Imeandaliwa na Abdallah Simba
0714222345

No comments:

Post a Comment