Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars),leo kimethibitisha kuwa kuna tatizo katika mfumo mzima wa soka la Tanzania, baada ya kufungwa goli 2-1, timu ya taifa ya Msumbiji maarufu kama THE MAMBAS katika mchezo wa pili wa kuwania nafasi za kuingia kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CHAN.
Katika mchezo uliopigwa katika uwanja mkuu wa Taifa wa nchi hiyo, kikosi hicho kilikuwa kinahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuweza kusonga mbele kitu ambacho kilishindikana.
Shukrani za pekee kwa mshambuliaji hatari wa TP MAZEMBE , Mbwana Samatta baada ya kufunga goli pekee na la mwisho kwa michuano ya Stars ndani ya CHAN mwaka huu.
Kwa matokeo hayo basi,kikosi hicho kinachonolewa na Martin Nooij kimetupwa nje kabisa na inafanya warudi nyumbani vichwa chini.
Wakati huo huo, kocha mkuu wa timu hiyo mholanzi Martin Nooij,amewalalamikia waamuzi kwa kuchezesha nje ya sheria 17 zinazosimamia mchezo huo.
Hii Si mara ya kwanza kwa Stars kufungwa na msumbiji kwani katika mechi 5 za mwisho kukutana, Stars kafungwa mara 3 na kutoka sare mara 2.
No comments:
Post a Comment