ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, August 6, 2014

UINGILIANO WA MAJUKUMU BADO TATIZO KATIKA VILABU VYETU

Moja ya kitu ambacho si kizuri katika soka la Tanzania basi ni uingiliano wa ugawanywaji wa majukumu.
Ugawanyaji wa majukumu hufanya kila kitu kiende sawa na kwa mpango sahihi. Ugawanywaji huu wa majukumu hauwezi kuukwepa hata kwenye klabu zetu mathalani Simba SC.

Ili klabu yoyote ifanye vizuri inahitaji umoja wa kweli, siku zote umoja wa kweli hujengwa kwa kushirikiana.

Sio siri tena katika viungo muhimu ndani ya klabu ya Simba SC ni ,mashabiki/wanachama/wapenzi /wachezaji, viongozi pamoja na kocha, ukiiharibu eneo lolote kati ya viungo hivyo basi utaumia tu

MASHABIKI/WAPENZI/WANACHAMA

Hawa mara nyingi ndio huumia sana pale timu inapofanya vibaya, bahati mbaya wengi wao hawajui kazi yao halisi ni ipi,
Kati yao huingilia sana maamuzin ya makocha na hata viongozi,wengine hufikia hatua hata ya kutukana baadhi ya wachezaji kana kwamba si wachezaji wao,mbaya zaidi kuna mashabiki wenye jinsia ya kike huingia ndani zaidi kwa wachezaji ili kutimiza wanachokihitaji,tatizo ni dogo tu hapa, inawezekana kuwa hawajitambui au sio mashabiki wa kweli,,

kundi hili linahitaji marekebiso ya hali ya juu kabla ya hali kuwa mbaya zaidi!

VIONGOZI

Mara nyingi tatizo huanzia hapa ila mashabiki hawafahamu au hawataki kufahamu kuwa tatizo huanzia haps,.
Kwanini nasema tatizo huanzia hapa?
Jibu ni ahisi tu, kwasababu hawa ndio walezi muhimu wa timu,hawa ndio wahusika zaidi wa wachezaji na hata wanachama.

Bahati mbaya baadhi yao wanakuwa 'kazini' kwa sababu ndicho wanachokifikiria, hii husababisha wale waliokuwa wanafanya kazi kwa kufata misingi ya soka kuonekana si mali kitu na yawezekana hata kuonekana si watu wazuri,

mfano; Kiongozi anapoingilia kazi ya kocha au hata kazi ya meneja wa timu, nini maana ya kuwa na kocha, au nini maana ya kuwa na meneja? hii si sahihi.

Kiongozi unapoingilia kazi ya shabiki eti mchezaji fulani hafai wakati yeye mwenyewe ndiye kampendekeza nini maana yake,, hii haifai, inahitaji kukemewa na ipo katika vilabu karibu vyetu vyote.


WACHEZAJI

Bahati mbaya wachezaji wetu wengi sio waelewa, wachezaji wetu wengi hupenda kudeka sehemu ambazo hawahitaji kudeka, wachezaji hujenga urafiki wa karibu sana ambao sio wa kikazi na baadhi ya viongozi hali inayopelekea kuharibu kazi muda mwingine.

Ili timu iweze kucheza mpira, mchezaji ndio muhusika mkuu, hivyo hana jinsi kufanya kazi kutokana na makubaliano na wajibu wake,

Ni jukumu la kila mtu kufanya kazi kwa nafasi yake ili tuweze kuwa bora zaidi,

Salaam!


No comments:

Post a Comment