Straika wa kimataifa wa timu ya taifa ya Kenya ambaye anakipiga katika timu ya KCB ya nchini humu Paul Kiongela,anataraji kutua nchini leo kujiunga na miamba ya soka ya Tanzania Simba SC.
Akiongea kwa njia ya simu mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili(jina linahifadhiwa), amesema kuwa ujio wa mshambuliaji huyo unafanywa kimya kimya ili kuweka mambo sawa zaidi kwa kuwa wanahofia uwenda wakazungukwa.
Paul Kiongela, ni mmoja wa washambuliaji safi kabisa afrika mashariki na ujio wake unasubiriwa kwa hamu kubwa, huku kocha wa Simba SC akimuweka katika listi ya wachezaji anaohitaji kufanya nao kazi msimu huu.
Wakati huo huo, timu ya soka ya Simba SC imeingia kambini tayari kabisa kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment