ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 2, 2014

TAMBWE AZIDI KUIMARIKA,ATUMA SALAAM KWA STAND UNITED

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayekipiga katika timu ya Simba SC Amissi Tambwe amesema kuwa anazidi kuimarika baada ya jana kuumia mazoezini alipogongana na beki Abdi Banda.

Mfungaji huyo wa zaidi ya magoli 18 msimu uliopita na kushinda tuzo ya ufungaji bora,amesema kuwa hali yake inazidi kutengemaa na Simba SC itarajie makubwa toka kwa timu yao.

Akiuzungumzia mchezo wa  kesho dhidi ya Stand United, Tambwe amesema kuwa yuko vizuri na amewaahidi wanasimba wafike kwa wingi kwani watafanya vizuri zaidi." tumejipanga, tumegundua wapi tulikosea na kesho ni imani yangu tutacheza soka la kuvutia na la ushindi ili tuwape furaha fans wetu"

Simba SC, kesho inatupa karata yake ya tatu katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare mbili mfululizo katika mechi mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment