ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, February 5, 2015

TFF INAPOAMUA KUIFANYA YANGA IWE TIMU YAKE


Haya ni maduud mengine ya Mzee Malinzi.Leo Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limemtangaza rasmi Baraka Kizuguto kuwa Afisa Habari wake.Taarifa zilizotolewa juu juu na bila ya kutangazwa wazi kwa wadau kujitokeza kugombea nafasi hiyo ya uafisa Habari TFF.Kwa ghafla wadau wa soka wamesikia jina la Baraka Kizuguto akitajwa kama Afisa Habari mpya wa TFF kuanzia Februari 1 mwaka 2015.Kwa Baraka inawezekana ni Baraka kubwa kama jina lake na pia ni bahti ya mtende kuotea juani.Lakini kwa wapenda soka lazima tuwe na mashaka jinsi mchakato mzima wa kumpata Afisa Habari ulivyofanyika katika njia za mashaka mpaka kupatikana Afisa Habari Baraka Kizuguto.Hofu yangu ni baada tu ya kusoma wasifu wa Baraka Kizuguto na kushuhudia kuwa Baraka mwenye miaka 33 amewashinda wenzake 10 ambao hawakutajwa majina yao na wasifu wao ktk tasnia hiyo.Ila Baraka ambaye amemaliza shule ya Msingi Amani mwaka 1996 amesoma pia sekondari y Bihawana kuanzia mwaka 1997-2000 kisha elimu ya juu akapata chuo cha PEC kuanzia mwaka 2002 mpaka 2003 na kwa mwaka huo mmoja akatunukiwa Cheti cha juu cha mafunzo ya Uandishi wa Habari na Masuala ya Umma kabla ya kusomea kinachoitwa "International Diploma in Computer Science toka pale chuo cha NCC kuanzia mwaka 2007-2009.Uzoefu ulioanikwa wa Baraka ktk kuongoza ni kuwa alikuwa Ofisa wa Lugha na Mawasikiano wa CHAVITA (sina uhakika ni kitu gani),Akawa kwa kazi ya muda TPa kama mtaalam wa kompyuta kwa miezi 7 tu kabla ya kuhamia kampuni inayojiita Susneirkers Group na kuwa mtaalam wa IT na Tovuti.Baada ya hapo kuanzia mwaka 2012 akawa mmoja wa watu wa utaalam na tovuti ktk klabu ya Yanga.Huo ndio wasifu wa Baraka ambaye ktk michezo hakuna hata sehemu iliyoripotiwa kufanya kwake kazi kwa ufanisi zaidi la Tanzania.Lakini leo bahati imemuangukia kawa msemaji wa TFF.Tusubiri tuone na tusikie kuhusu uwepo wa sheria 21 za akina Jerry Muro zitakazoanza kutolewa na Baraka.TFF nilidhani wangetafuta mdau aliyesomea na kufahamu vema masuala ya michezo na sheria zake lakini mtu aliye na elimu bora toka vyuo bora vya elimu hiyo ya uandishi wa habari na sio kuwa kimbilio la makanjanja wa vyeti visivyo na ubora.Tutegemee kuona magumashi kadha wa kadha siku chche zijazo.Nadhani kwa kuwa TFF wana Mkutano wao wa Kawaida utakaofanyika mwezi ujao wa Machi kuanzia tarehe 14/15 basi ni muda mwafaka kwa wajumbe wa mkutano huo kumbana kiongozi wao Mkuu Jamaal MalinI juu ya "Masihara" anayoendelea kutuletea ndani ya soka la Bongo.

No comments:

Post a Comment