ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, September 26, 2013

Kaseja kurudishwa kundini iwapo............


Goli kipa nguli wa zamani ambaye alifungashiwa virago vyake Simba SC Juma Kaseja , huenda akarudishwa kundini katika dirisha dogo la usajili.
Hii imekuja wiki kadhaa baada ya kuonekana udhaifu na uwezo mdogo wa kipa wake namba mbili Andrew Ntalla.
Juma Kaseja aliachwa Simba Sc huku ikisemekana kuwa kiwango kimeshuka lakini wengine walienda mbali zaidi na kusema kuwa anaigawa timu yeye akiwa kama nahodha.
Kwa sasa Simba SC ina makipa wawili tu ambao wanaonekana wako kikazi zaidi , Abel Dhaira na Abuu Magube huku ikisemekana Andrew Ntalla hataki wala kuzisikia mechi za kimashindano kiasi cha kwamba akiambiwa asimame katika milingoti mitatu hujifanya anaumwa ili asiweze kucheza kwa muda huo

No comments:

Post a Comment