ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, September 28, 2013

ZAHORO PAZI, Fundi wa mpira anayeweza kujipoteza kama asipobadilika

Miongoni mwa vitu vinavyowashangaza sana kwa sasa mashabiki wa Simba ni kutokuona ingizo lililosajiliwa msimu huu la Zahoro Pazi.
Ukiimgia kichwa kichwa unaweza kusema kuwa Abdallah Kibaden anamuonea kijana huyu kwani hata muda mwingine kwenye benchi pia huwa hayupo, lakini si kweli.
Msimu huu timu ya Simba imesajili wachezaji vijana wenye ndoto za kufika mbali wengi sana, kitendo cha uongozi wa Simba kuwapandisha vijana wa timu B ambao ni mabingwa wa muda wote wa michuano ya ABC super 8 ni kitendo cha kupongezwa sana, vijana hawa wenye ushindani wa hatari uwanjani ndipo mpira halisi wa Zahoro Pazi umefichwa, mara nyingi huwa nakwenda sana mazoezini na kuangalia jinsi timu yangu ninayoipenda kwa dhati inavyocheza, hakika mpira mwingi huwa unapigwa kule ila kuna wachezaji wana kazi kubwa sana kupata namba, miongoni mwa wachezaji hao ni huyu Zahoro Pazi ambaye mpira wake mwingi husikiza mashabiki au huwa na maamuzi mengi sana kwa wakati mmoja kiasi cha kupelekea kuupoteza mpira kwa muda mwingi au kupokonywa na adui,.
Ni wajibu wake mwenyewe kutulia na kutokuwa na papara pia achukulie Simba ni kama njia tu ya kuelekea kule kuliko bora kuliko Simba, hakuna asiyefahamu uwezo binafsi wa huyu jamaa ila kuzidiwa na uwezo mkubwa wa akina Chanongo na Ndemla kunamfanya afanye kazi ya ziada.
Naamini atabadilika na kuwa katika ubora wake uliozoeleka siku zote.

No comments:

Post a Comment