ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, September 28, 2013

SIMBA VITANI DHIDI YA JKT RUVU LEO

Timu ya soka ya Simba SC , leo inatarajiwa kushuka dimbani katika uwanja wa Taifa kucheza na timu ya jeshi la Tanzania JKT Ruvu.
Ikiwa imekwishajikusanyia pointi 11 huku ikichanja mbuga katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, Simba italazimika kupambana kiume ili kuweza kupata pointi 3 muhimu kwani ina kumbukumbu mbaya ya kuambulia pointi moja katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, viungo Henry Joseph, Jonas Mkude na beki ya kushoto Idrissa Rashid wataukosa mchezo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za majeraha na kadi.
Wakati Idrissa Jonas Mkude akiukosa mchezo wa leo kwa kuwa ana kadi 3 za njano, Henry Joseph atakuwa nje kwa kuwa ni majeruhi kama ilivyo kwa mwenzake Idrissa Rashid ambaye alipata majeraha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ndanda FC.
Hii ina maana kocha King Kibaden anaweza akaingiza ingizo jipya la beki ya kushoto ambaye ni Adeyoum Saleh huku dimba la kati likitegemewa kukamatwa na Said Ndemla au Abdulhalim Humud.
MUNGU IBARIKI SIMBA SC




No comments:

Post a Comment