ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, November 30, 2013

Kocha mpya Simba kuwasili kesho

Kocha mpya wa Simba Sc Zdravko Lugarusic anatarajia kuwasili kesho majira ya saa 2.00 Asubuhi kujiunga na timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Croatia , anatarajiwa kusaini mkataba wa Miezi Sita ili kukifundisha kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Kabla ya kutua Simba, Lugarusic aliwahi kukinoa kikosi cha Gormahia ya Kenya , na kukiwezesha kuchukua Kombe la ligi kuu nchini humo,.

Huyu atakuwa kocha mkuu wa pili wa Simba msimu huu, baada ya kutimuliwa kwa aliyewahi kuwa kocha wa Simba Bw Abdallah Kibaden Mputa.

No comments:

Post a Comment