ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, November 30, 2013

SABA ZAIDI KUSITISHIWA MIKATABA YAO SIMBA SC

Baada ya kutoka taarifa za kusitishiwa mkataba wa aliyekuwa mchezaji wa Simba Sino Agustino ,  taarifa za ndani kabisa ya Klabu hiyo zinasema kuwa zaidi ya wachezaji Saba wa Simba watakumbana na rungu hilo.

Hii imethibitishwa na mmoja wa miongoni wa wajumbe wa kamati ya utendaji( Jina linahifadhiwa)baada blog hii kupata taarifa kuwa wachezaji hao Saba mikataba Yao itasitishwa.

Wakati Huohuo, aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Sc Bw Jamhuri Kihwelo Julio, amemshambulia kwa maneno makali mwanachama wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu, na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Ibrahim Masoud, kwa Madai ya kuwa wao wanahusika moja kwa moja kwa yeye kusitishiwa kibarua chake na Simba Sc.

Akiongea kwa hasira na kujiamini Jana wakati akihojiwa na vyombo vya habari, Bw Julio amesema kuwa anatambua kuwa Kaburu Ndiyo aliyefanikisha mpango huo wa yeye kuondoka alishirikiana na Maestro ( Ibrahim Masoud) Huku akithibitisha Baadhi ya wachezaji aliyowasajili yeye , wameshapewa barua rasmi za kusitishiwa mikataba Yao kwa sababu asizozijua.

Wakati vita ya kamati utendaji ya Simba Sc na makocha wao wa zamani ikiendelea , kocha mpya wa Timu hiyo Zdravko Lugarusic , anatarajiwa kuwasili Leo hii majira ya saa 2.00 Asubuhi kwa ndege ya Shirika la Kenya yaani Kenya Air ways.

No comments:

Post a Comment