ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, November 28, 2013

SIMBA KUANZA MAZOEZI DEC MOSI

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar Es Salaam, inatarajiwa kuanza mazoezi rasmi Dec mosi, katika kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tabzania bora.


Timu hiyo kutoka Mitaa ya Msimbazi, inatarajiwa kuwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola ( Veron) ambaye amepewa kibarua hicho baada ya kusimamishwa kwa makocha wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibaden na mwenzake Jamhuri Kihwelo Julio, kutokana na Mwenendo mbovu wa timu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara.


Wakati huo huo, kocha atakayerithi mikoba ya Abdallah Kibaden Zdravko Logarusic , anatarajia kuwasili Dec 1, baada ya kutumiwa tiketi na kamati ya utendaji ya Simba.

No comments:

Post a Comment