ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, November 18, 2013

SIMBA YA MATOLA KIBOKO,YAISHINDILIA OLJORO 3-0

Ibrahim Hajib (BOBAN),jana alikuwa kinara wa maangamizi ya Simba B dhidi ya Jkt Oljoro katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mabao ya kinda hilo ya dakika za 26 na 43, na lila la Miraji Athuman Dakika ya 47, yalitosha kabisa kupeleka kilio katika kambi ya wanajeshi  hao wa jijini Arusha.

Ikionesha soka safi na la kuvutia zaidi,timu hiyo inayofundishwa na nahodha wa zamani wa Simba ilionekana iko safi kila idara, huku chipukizi toka timu ya A sAID Ndemla,akionesha ukomavu wa hali ya juu.


Kikosi cha Simba kilikuwa ni
Abuu Hashim
Miza Abdallah
Emily Mgeta
Hassan Isihaka
Carlos Potas
Said Ndemla/Sultan Shija
Mohamed Salum/Jesse Nyombo,
Issa Abdallah
Ibrahim Hajib(Boban)
Miraji Athuman
Abdul Salum

No comments:

Post a Comment