ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, December 16, 2013

EDO KUJIUNGA NA WENZAKE LEO HII

Mshambuliaji bora wa michuano ya Banc ABC SUper 8 Edward Christopher ' EDO' , anatarajia kujiunga na wenzake Leo hii baada ya Jana kushindwa kusafiri na wenzake .

Kinda hilo lililojizolea umaarufu baada ya kufanya kazi safi katika michuano ya benki ya ABC BAnc, anatazamiwa kuondoka Leo na boti ya saa 6. 00 mchana kuelekea visiwani humo kukiongezea nguvu kikosi cha Simba kinachojiwinda na michuano ya Mapinduzi itakayofanyika visiwani humo.


Wakati Huohuo , wachezaji wapya waliokuwa wamesajiliwa msimu huu wameungana tayari na wenzao kukamilisha kikosi kazi kitakachotoa adhabu kali kwa watani wao Yanga siku ya jumamosi!

Wachezaji hao ambao walikuwa Kenya kwenye timu zao za taifa ni Issa Machete na Ally Badru wanaotokea timu ya taifa ya Zanzibar , Donald Musoti anayetokea upande wa Kenya na Tanzania one kwa sasa Ivo Mapunda ambaye anarithi mikoba ya Abel Dhaira aliyetupiwa virago vyake!

No comments:

Post a Comment