ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, January 23, 2014

RAIS BARCELONA ATAKA KUJIUZURU


SOCCER-SPAIN/BARCELONAZIMEIBUKA ripoti huko Spain kuwa Rais wa FC Barcelona, Sandro Rosell, amewasilisha uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake.Inadaiwa Rosell alilipua uamuzi huo wakati alipotembelewa na Josep Maria Bartomeu na Javier Faus, ambao wote wawili ni Makamu wa Rais wa Barca.

Hata hivyo, Usiku huu kipo Kikao cha Dharura cha Bodi ya Klabu ambacho kitajadili nini mustakabali wa Klabu kufuatia kutinga Mahakamani wakichunguzwa kwa Ubadhirifu wa Fedha kwenye Uhamisho wa Supastaa wa Brazil Neymar kutoka Santos kwenda Barca mwanzoni mwa Msimu.

clip_image001Tuhuma dhidi ya Barca na Rosell ni gharama halisi za Uhamisho wa Neymar ambao Barca walitangaza kuwa ni Uhamisho wa Dau la Euro Milioni 57.1 wakati yapo madai ni zaidi ya hapo na yapo malipo ya siri yaliyofanyika.

Kesi hii, itasikilizwa na Jaji Pablo Ruz ambae anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa Ushahidi.

Kesi hii inafuatia malamiko ya Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ameungwa mkono na Waendesha Mashitaka wa Spain waliokubaliana na Madai yake kwamba kulikuwepo ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki.

Pia, wametaja Kitita cha Euro Milioni 40 kilicholipwa kwa Kampuni ya Baba yake Neymar ambacho hakikutangazwa katika Uhamisho huo.

Juzi Jumatatu, Gazeti maarufu huko Spain, El Mundo, lilitoboa kuwa Dau halisi la kumnunua Neymar ni Euro Milioni 95 kitu ambacho kilimfanya Rais Sandro Rosell atake nafasi Mahakamani ili atoe ushahidi na kujisafisha.

Hiyo Jumatatu, Rosell, akiongea na Wanahabari alitamka: “Kuna vitu viwili nataka kusema. Kwanza Neymar aligharimu Euro Milioni 57.1. Na hili nimesema mara nyingi. La pili, ni ombi, kwa heshima namuomba Jaji aniite ili nitoe ushahidi na kumwambia kila kitu anachotaka kujua kwa sababu hamna cha kuficha!”

Katika kuisikiliza Kesi hii, Jaji Pablo Ruz anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa Ushahidi.

Rosell alishinda Uchaguzi wa Rais wa Barca Mwaka 2010 na alitakiwa ashike wadhifa huo hadi 2016 lakini sasa Nafasi hiyo itakamatwa na Bartomeu hadi Uchaguzi ujao.

No comments:

Post a Comment