Mfungaji bora wa klabu bingwa afrika mashariki na kati na ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita Amissi Tambwe ameanza mazoezi mepesi.
Tambwe ambaye anajulikana kwa jina la 'goal master' ameamua kuanza mazoezi hayo ili aweze kujiweka fiti zaidi kabla ya kuanza kwa mtanange wa ligi hiyi unaotarajiwa kuanza mwezi agosti.
Wakati huo huo, stopa ya timu ya taifa ya Burundi na klabu ya Simba Gilbert Kaze huenda akapelekwa kwa mkopo katika timu ya coastal Union ya jijini Tanga.
Kaze amekuwa mtu wa kusugua benchi tangu kufika kwa Beki wa timu ya taifa ya Kenya Donald Musoti.
No comments:
Post a Comment