ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, June 10, 2014

WAMBURA YAMETIMIA

Mgombea urais wa Simba Sc Michael Richard Wambura huenda akaendelea kuwania urais baadaya ya kushinda rufaa yake.
Taarifa ilizozinasa kutoka katika kikao hicho kizito zinasema kuwa, wakata rufaa wote na mkatiwa rufaa waliweza kushinda hoja zao kwa uhakika zaidi.

Habari zinaendelea kusema kuwa baada ya kuwa sawa kwa hoja ndipo kamati ya rufaa iliamua kupiga kura ya vidole hali iliyopelekea Bw Wambura kupata kura 3 dhidi ya 2 za waliotaka aondolewe.


Blogu hii ilimpigia simu moja kwa moja msemaji waTff Bw Boniface Wambura ambaye alijibu kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa atatoa taarifa rasmi leo majira ya saa tano kamili asubuhi.

No comments:

Post a Comment