ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, August 29, 2014

CASSILAS AREJEA MANUNGU KUWAUA MTIBWA SUGAR

Kipa mpya wa Simba SC Hussein Sharrif (Cassilas ) anatarajiwa kurejea dimbani kucheza na timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

Kipa huyo aliyeshinda tuzo ya goli kipa bora wa ligi kuu Tanzania bara misimu miwili mfululizo,anarejea katika mchezo huo wa kirafiki utakaopigwa Septemba 6.

Simba SC, inatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar katika mechi ambayo inatarajiwa kuwa nzuri na ya kusisimua.

Wakati huo huo,kiungo ambaye alitarajiwa kupelekwa kwa mkopo katika timu ya Stand United Awadh Juma amerudishwa kundini.
Tayari mchezaji huyo amejiunga na timu yake ya Simba SC ,iliyoweka kambi katika visiwa vya unguja.

No comments:

Post a Comment