ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, October 3, 2014

NDEMLA: STAND NI WAZURI ILA WANACHEZA DHIDI YA SIMBA KATIKA KIPINDI KIBAYA

Kiungo wa kutumainiwa wa Simba SC Said Ndemla amesema kuwa ni ushindi tu ndio utakofanya morali ya vijana wa Simba SC kurejea.
Akiongea na SPS blog baada ya kumaliza mazoezi yaliyofanyika jana, Ndemla amesema kuwa tuko imara na tunaenda kupambana kwa ajili ya bendera ya Simba SC." Ni kweli tulianza vibaya ila naamini kocha wetu amefanyia kazi, tunahitaji pointi tatu toka kwao kama wao wanazohitaji toka kwetu, natoa angalizo wasitegemee mechi rahisi" aliongeza.

Simba SC inaivaa Stand United leo huku ikiwa na mwanzo ambao si wa kuridhisha baada ya kupata sare mbili mfululizo.

Wakati huo huo, Rais wa Simba SC Evance Elieza Aveva amesema kuwa huu si wakati wa wanasimba kuisusa timu yao, akizungumza muda mfupi baada ya kuhudhuria mazoezi ya vijana wake, Evance amesema kuwa Simba ni timu kubwa na wao kama viongozi wanatambua umuhimu wa ushindi." tumejipanga kujua tatizo ni nini, nna imani mwalimu atayafanyia kazi na kuwa na muendelezo mzuri" alisema

No comments:

Post a Comment