ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, January 14, 2015

KISIGA; HAJIB SI WA KUCHEZA TANZANIA

Uwezo unaoendelea kuonyeshwa na kiungo chipukizi wa Simba, Ibrahim Ajibu, umemkuna kiungo wa timu hiyo, Shaban Kisiga na akatamka wazi kuwa mchezaji huyo si wa kuendelea kuwepo kwenye ligi ya Tanzania kwa muda mrefu.


Ajibu ambaye amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Polisi Moro, amekuwa gumzo kwa sasa, hasa baada ya kufanikiwa kuonyesha kiwango cha kuvutia kwenye Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar.

Kisiga alisema kuwa Ajibu si mchezaji mwenye uwezo wa kawaida bali ni mchezaji anayefahamu soka kiuhalisia, hivyo mchezaji kama huyo anapaswa kufikiria kucheza soka la kulipwa mapema mno na si kuendelea kuwepo kwenye ligi ya Bongo.

“Ni mchezaji mzuri, anavutia sana akiwa anacheza mpira, mchezaji kama huyo hastahili kuendelea kuwepo hapa Tanzania kwa muda mrefu, hawa ni watu wa kucheza nje ya nchi soka la kulipwa, anatakiwa kuangalia zaidi nje kuanzia sasa na si kuendelea kuzunguka katika timu za Tanzania.


“Lakini pia kama akijitunza na kujithamini, akizipuuzia anasa na mambo mengine yasiyo na msingi, akifuata misingi ya soka, naamini atafika mbali zaidi,” alisema Kisiga.

No comments:

Post a Comment