ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, January 16, 2015

KOPUNOVIC ATUMA SALAAM KWA WACHEZAJI HAWA SIMBA SC



Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ametangaza mapemaa kwamba aina tatu za wachezaji hawawezi kudumu katika kikosi chake.

Kopunovic raia wa Serbia amesema wachezaji wasiotaka kujituma ndiyo kundi la kwanza hawatakuwa na nafasi katika kikosi chake.
“Pili ni wale wasiokuwa na nidhamu na tatu wasiocheza kwa manufaa ya timu au kuangalia manufaa ya pamoja kama timu, hakika hawawezi kukaa na mimi,” alisema Kopunovic.

“Mimi naamini katika kukosea, lakini nisingependa kuona mtu asiye na nidhamu au asiyejituma au mbinafsi anaangalia maslahi yake, hawezi kuwa na nafasi kabisa.”

Kopunovic alisema kwa kuwa anaamini katika kukosea kwamba binadamu anapokesea na kurekebisha makosa yake anakuwa bora zaidi, basi yuko tayari kuvumilia mambo mengi.

“Si lahisi kwa kosa moja ukaamini mtu ana matatizo, wote tunakosea lakini anayerudia kukosea kila mara anakuwa si mtu mzuri,” alisisitiza.

Kocha huyo atakuwa na mtihani wake wa kwanza wa ukweli wakati atakapoingoza Simba katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.

Simba itakuwa inacheza mechi yake ya tisa ikiwa ugenini dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara lakini itakuwa ni mechi ya kwanza ya Mserbia huyo.

Kabla ya hapo, Simba imecheza mechi nane chini ya Mzambia Patrick Phiri, ikashinda moja, sare sita na kupoteza moja.
Imehamishwa toka kwa Saleh Ally

17Jan
2015

No comments:

Post a Comment